Kuepuka wizi haramu

Skip listen and sharing tools

Wizi haramu ni hila zilizotengenezwa na watu wasiokuwa waaminifu kuiba fedha yako au maelezo ya binafsi.

Wezi haramu wanaweza kutumia simu, barua pepe, ujumbe wa maandishi na barua ili kuwasiliana na watu. Hapa chini ni baadhi ya maelezo ya kukusaidia kutambua na kujikinga na aina tatu za wizi haramu wa kawaida.

Wizi haramu wa mchezo wa bahati na sibu

Wezi haramu hutuma barua inayofanana na halisi, barua pepe, ujumbe wa maandishi au vyombo vya habari vya kijamii wakikwambia kwamba umeshinda tuzo. Tuzo inaweza kuwa fedha, likizo, smartphone au vocha ya manunuzi. Kudai zawadi, wanasema lazima kwanza ulipe kodi au ada, au uwatumie maelezo ya akaunti ya benki yako.

Baadhi ya alama za tahadhari za wizi huu haramu zinajumuisha:

  • zawadi ni kwa ajiri ya bahati na sibu au mashindano ambayo hukuyaingia
  • unaombwa kupiga simu au kutuma barua pepe ya maelezo yako binafsi
  • ni lazima utume gharama au taarifa zako za benki ili uweze kudai zawadi yako
  • namba yako ya posta, barua pepe au namba ya simu inatolewa kama taarifa za mawasiliano (hakuna anwani ya mtaa inayotolewa).

Wizi haramu wa msaada

Wezi haramu wanajifanya kuwa wanatoka serikalini,benki au shirika linguine linalojulikana na kusema kuwa unawadai pesa - lakini lazima kwanza ulipie gharama za uendeshaji au gharama zinazofanana ili 'kulipwa'. Baadhi ya wezi wa haramu husema pia kuwa pensheni yako au posho haikulipwa yote, au bili ya umeme ililipwa kubwa kama sababu ya kutaka urudishiwe.

Benki ya kweli, biashara au idara ya serikali haitaweza kuwasiliana nawe na kusema kuwa unaidai harafu ikutake ulipe pesa ya ziada.

Wizi haramu wa mapenzi

Wezi haramu wanawafikia walegwa kupitia tovuti za mapenzi. Baada ya kuwa mapenzi yameanza kukua, wanahamisha taarifa za mawasiliano zote kwenye parua pepe binafsi, kupiga simu au ujumbe wa papo hapo. Baada ya mda, mwizi haramu anajenga uhusiano wa kwenye mtandao pamoja na mlengwa, kwa kwenda mbali ili kuweza kuaminiwa na upendo.

Hatimaye, mwizi haramu hufanya hadithi ya kutaka umpe fedha, mara nyingi akisimamia ugonjwa au kuumia kwa familia, au kulipia mtaji wa uwekezaji. Katika hatua hii, mwathirika anakujwa ameshajitoa kwa ajiri yao hivyo kuweza kutuma pesa kwa urahisi, hata kama ndugu wa familia na rafiki akimwambia kuwa ni wezi haramu. Baada ya kuwa pesa imeshatumwa kwenye mtandao au njia za kusafirisha pesa, ni vigumu sana kuweza kuirudisha.

Kujilinda mwenyewe - vitu vya muhimu vya kuzingatia kuhusu wezi haramu

  • kama inaonekana kuwa kweli basi inaweza kuwa kweli
  • kuwa waangalifu sana a barua pepe zenye mashaka, simu au barua zinazosema kuwa una fedha unayodai au una deni nao
  • usije ukatuma pesa au taarifa za benki yako ili eti uweze kupata msaada
  • tazama kama uliingia kwenye mashindano ya bahati na sibu au mashindano ya zawadi na kumbuka kuwa bahati na sibu halali haitakuuliza kulipia gharama ili upate zawadi au ushindi
  • usilipia chochote kile kwa njia ya mtandao au usafirishaji pesa - mda wote tumia njia nzuri kama vile kadi ya Credit au PayPal
  • fahamu tovuti za bandia ambazo zinaonekana kuwa na nembo nzuri kama halali za benki zinazojulikana au mashirika mengine - kama huna uhakika, wasiliana na benki au shirika husika moja kwa moja
  • usitumie miongozo ya kwenye barua pepe kuwasiliana na biashara husika. Mda wote tafuta habari za mawasiliano ukitumia injini za kutafutia, mwongozo wa simu au chanzo kingine kinachojitegemea
  • usije ukatuma pesa kwa mtu ambaye hamujawahi kukutana uso kwa uso, hata kama umeshazungumza nao au kupokea zawadi kutoka kwao
  • sikiliza familia na marafiki kama wana wasiwasi kuhusu huyu mtu mliyekutana naye kwenye mtandao
  • uwe makini kama picha ya kimapenzi ya kwenye mtandao haiendani na maelezo au kufanana na ile iliyokamatwa kwenye magazeti.

Kuchukua hatua kuzuia wezi haramu

Kama unafikiria kuwa unaweza kuwa umeibiwa kiharamu, wasiliana nasi mara moja ukitoa taaria hiyo. Kutegemeana na mazingira yako, unaweza kuweza kurudishiwa pesa kupitia shirika la kadi yako ya credit au banki.

Kama huwezi kurudishiwa pesa yako, bado ni muhimu kutoa taarifa, maana habari zako zinaweza kutusaidia kuzuia wengine kuweza kuibiwa kiharamu.

Jifunze zaidi jinsi ya kukwepa wizi haramu kwa kutazama video yetu ya Stevie’s Scam School videos kwa watumiaji na wafanyabiashara wadogo.