Kuuza mlango kwa mlango

Skip listen and sharing tools

Haki yako hapa Australia.

Nini kuuza mlango kwa mlango?

Kuuza mlango kwa mlando ni pamoja na watu:

 • wanajaribu kuuza vitu vya nyumbani
 • wanakubari kutengeneza nyumba yako
 • wanakuomba kubadirisha gesi, umeme, simu au mtowaji wa intaneti.

Lini muuzaji anakuja kwenye mlango?

Muuzaji anaruhusiwa kuja kwenye mlango katika:

 • 9:00 am na 6:00 pm juma tatu na ijuma
 • 9:00 am na 5:00 pm juma mosi.

Hawawezi kuja ijuma pili au siku za likizo ya umma.

Hata hivyo, muuzaji anaweza kutembelea wakati wowote akiwa na makubaliano yako.

Sheria gani muuzaji wa mlango kwa mlango anapashwa kufuwata?

Wakati anakuja kwenye mlango wako, muuzaji lazima:

 • wakwambie kwanini anakutembereya
 • wakwambie majina yawo na shirika wanatumikiya
 • wakwambiye kwamba watatoka kama unawambia hivo (kama naambia muuzaji atoke, hawawezi kukuita tena angalau kwa wakati wasiku 30)
 • wakwambiye haki yako ya kuacha makubaliano (hii ikiwemo namuna ya kufuta makubaliano)
 • pamoja na maelezo kamili ya kuwasiliana na makubaliano yoyote ya saini kwa niaba ya wasambazaji wao
 • kukupa nakala ya maandishi ya makubaliano yoyote kabla imesainiwa
 • kutokuuliza kwa ajili ya malipo ndani ya siku 10 ya kutia saini kwenye makubaliano
 • kutotoa bidhaa vya bei zaidi ya $500 ndani ya siku 10 ya kusaini makubaliano
 • kutotoa huduma ndani ya siku 10 ya kutia saini mkataba huo.

Kama sipendejwi navitu muuzaji iko anatowa - naweza kufanya nini?

 • Kusema ‘hapana aksante’.
 • Usihisi unasukumwa kununuwa chochote kutoka kwenye mtu anakuja ku mlango wako.

Kila siku sema ‘hapana’ kama muuzaji:

 • anatoa bei ambao inasikika kuwa ya kweli kwako
 • anakuuliza pesa kabla yakukupatia vitu au huduma
 • anatabia katika njia ambayo inakufanya ukasilike au unakuwa na wasiwasi.

Watu wanajifanya wanatoka mu selikari

 • Mtu anaweza kuja kwenye mlango wako nakusema kwamba anatoka selikarini- kwa mfano kwenye offisi ya kodi ya Australia au Centrelink.
 • Wanakuuliza namba za benki yako au habari binafsi zako, kwa mfano kulipa kodi, kupandisha malipo yako ya Centrelink.
 • Wanaweza kutumiya hizo habari kuiba fedha zako au kitamgulisho.

Kumbuka: kuwa makini kama mtu anakuja kwenye mlango wako na kusema kwamba anatoka selikari. Kila siku omba kitambulisho. Kesi nyingi, selikari hayiwasiliyani nawe namna hiyo.

Nimepandezwa na vitu muuzaji anaweza kutoa ... nifanye nini?

Kama unasema ndiyo kununuwa kitu kutoka kwa muuzaji, utaulizwa kusaini makubaliano. Makubaliano anapashwa:

 • kuandikwa katika lugha ya wazi
 • ni pamoja na masharti yote katika kamili
 • ni pamoja na bei ya jumla, au jinsi hii ni mahesabu
 • ni pamoja na madai yoyote ya posta au utoaji
 • vyenye jina na maelezo ya mawasiliano ya muuzaji
 • ni pamoja na maelezo wasambazaji ikiwa ni pamoja na anwani na maelezo ya kuwasiliana
 • saini yako na muuzaji
 • kuwa imeandikwa wazi au kuchapishwa (ingawa mabadiliko yoyote inaweza kufanywa kwa kalamu na saini)
 • yana habari kuhusu haki zako kufuta au kuacha mkataba
 • kueleweka kwa urahisi
 • kuwa na fomu ambao inaeleza haki yako kama wewe unabadili akili yako.

Kumbuka: kamahusemi kingeleza vizuri, siyo sahihi muuzaji kutumia mtoto wako kama mukalimani harafu usaini makubaliano. Kabla ya kusiani unapashwa kuomba kopi ya makubaliano ya lugha yako.

Nime saini makubaliano harafu nabadili hakili yangu ... naweza kufanya nini?

Kama anakubali kununua vitu au kupata huduma kwa fedha Zaidi ya $100 kwanjiya ya muuzaji wa mlango kwa mlango, una siku 10 siku za biashara yakubad ilisha mawazo kuhusu makubaliano. Uyo muda ni muda ambao unaweza kubadirisha mawazo yako, kwenye mda huyo, unaweza guchaguwa kuacha, unaweza kuacha kulipa.

Kabla ya kukubaliana, muuzaji lazima akujulishe kwamba una haki hii. Kama unabadilisha hakili yako wakati unakubarika kurudisha kitu ulicho nunuwa muuzaji haruhusiwi.

 • Kukuuliza 'kuondoa' mda huo wakudisha kitu kama kimeharibika
 • Kukusukuma ili useme ndiyo kwa makubaliano
 • Kukwambia kulipa pesa kwa ajili ya kufuta.

Unaweza kuacha makubaliyano kwa mdomo au kwa kuandika.

Mtu mwingine anakuja kwenye mlango wako na anakuomba mubadirishe gesi na umeme, wanakwambiyakwamba watatowa huduma nzuri na itasaidia kuzingatiya pesa

 • Wanakwambiyakwamba watatowa huduma nzuri na itasaidia kuzingatiya pesa.
 • Muuzaji anakuharikisha usaini makubaliano.
 • Unajihisi unasukumwa na kusaini.
 • Siku ifuwatayo, unaamuwa kutoshiliki.

Kumbuka:

 • usijisikii kushinikizwa kusaini mkataba, unaweza kuuliza muuzaji kuacha habari kwako kusoma
 • kama unasaini na unabadirisha akili yako, ungari una yule mda wakubadirisha mawazo yako
 • wasiliana na kampuni ya mauzo ndani ya siku 10 uwaambie kwanba umebadili akili yako
 • mauzo ya kampuni hawezi kukulipisha chochote kwa ajili ya kubadilisha akili yako.

Kwa maelezo juu ya mauzo ya mlango kwa mlango ambayo yanaweza kuwa si ya kweli, tembelea tovuti SCAM watch website.