Watu Wanaozungukia Nyumba

Skip listen and sharing tools

Watu wanaozungukia nyumba ni wafanyabiashara wezi ambao hubisha juu ya milango ya nyumba za kuishi na biashara ndogo ndogo, wakiomba kufanya kazi za matengenezo.

Wanaonekana mara nyingi zaidi wakati wa msimu wa joto na baada ya majanga ya asili, kama vile mafuriko, moto na dhoruba, wakati watu wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wanasafisha au kukarabati mali zao.

Watu wanaozungukia nyumba huomba kufanya kazi kama vile kutengeneza mifereji, uchoraji, matengenezo ya paa na kusafisha sakafu katika kiwango cha bei nafuu. Mara nyingi, hushinikiza watu, wakitoa punguzo la 'leo tu'.

Kwa nini unapaswa kuwaepuka?

Watu wanaozungukia nyumba huwa wanauliza fedha kabla ya kuanza kazi na mara nyingi kutoweka kwa haraka baada ya kuwalipa.

Kama wakifanya kazi yoyote, mara nyingi haimaliziki au ya kiwango cha chini.

Huwa wanatembea haraka na kwa kawaida hutoa jina la kwanza na simu ya mkononi - hivyo kuwasiliana nao baadaye inakuwa vigumu.

Kitu gani unapaswa kuangalia?

Uwe na wasiwasi na watu ambao:

  • bisha kwenye mlango bila kutazamiwa wakiomba kufanya:
    • kupaka rangi kwenye nyumba
    • kusafisha bustani yako au kukata miti
    • kutengeneza mifereji
    • kutengeza paa lako
  • kutoa mikataba ya bei nafuu kwa kutumia maneno kama 'kwa leo tu'
  • kuomba pesa kabla ya kufanya kazi
  • wakitoa msaada wa kukupeleka banki na gari ili kupata pesa za kulipa kwa ajili ya kazi
  • kukulazimisha ili ukubali kutaka kwao
  • wakisema wanaweza kufanya kazi sasa maana kazi nyingine kwa jirani imefutwa.

Kujilinda mwenyewe - mambo ya kuzingatia kujilinda na wanaozungukia majumba

Kama ukishtukia watu hao wanaozungukia majumba wakigonga, usiwajibu.

Kama ukizungumza nao, waombe kuondoka. Kama wakikataa kuondoka, wanavunja sheria.

Usite kupokea kutumikiwa kwa bei nafuu. Inaweza kugharimu zaidi katika muda ujao. Kama unataka kazi kufanyika kwenye nyumba yako:

  • fanya uchunguzi karibu yako kujua kadirio la gharama zinazokufaa
  • tumia mafundi wanaoweza kutoa kadirio la gharama kwa maandishi
  • omba namba za mawasiliano za mteja aliyetangulia ili uweza kuuliza uaminifu wa huyo mtu
  • usijaze mkataba wowote mpaka ukiwa tayari
  • uliza majina yote ya fundi huyo na kibali chake au leseni (kama inawezekana) unaweza kuangalia vitu hivi kutoka mamlaka ya idara husika.
  • uliza namba ya biashara, ili uweze kupiga kuhakikisha kama huyo fundi ni mfanyakazi wao.

Hasa baada ya majagwa, uwe makini na mtu yeyote anayetaka kufanya kazi 'leo tu' ili afanye matengenezo kwa pesa inayoonekana. Kwa ushauri katika majagwa, tembelea ukurasa wa lugha ya Kiingereza wa Advice in a disaster.

Kuchukua hatua kwa watu wanaozungukia majumba

Ili kutusaidia katika kutahadharisha jamii yako kuhusu hawa wezi wa mitaani, tafadhali weka miongozo kwenye ukurasa huu kwenye vyombo vya habari na anzisha maongezi katika Kiswahili. Kama unajua watu wanaozunguka majumbani katika maeneo yako:

  • weka kumbukumbu ya taarifa nyingi zinazowezekana, kama vile majina yao na zile za gari kuandikishwa
  • pigia namba za kitaifa kwa watu wanaozunguka majumbani (1300 133 408) kati ya 8:30am na 5:00pm Jumatatu hadi Ijumaa (isipokuwa siku za likizo)
  • toa taarifa kwa polisi wa mahali
  • tuandikie kwa Twitter mkato #stopconmen na tufuatilie kwenye @consumervic kupata habari mpya kuhusu mahali walipo watu wanaozunguka majumbani
  • andika ukurasa wa National Travelling Con Men Facebook kwenye facebook.com/StopTravellingConMen
  • listen to our information in Swahili:
Skip audio: tcmSwahili
Audio skipped