Haki yako kukodisha

Skip listen and sharing tools

Mwanzo wa upangaji

Kabla yakukodi nyumba, unahitaji kuwa na maandishi au maneno ya mkataba wa upangaji na kuwa na fedha za kutosha kulipa dhamana.

 • Mkataba wa upangaji (pia iitwayo makbaliano ya kukodisha) ni mkataba kati ya wewe na mwenye nyumba yako. Inasema kodi, dhamana, urefu na aina ya upangaji na masharti mengine na sheria.
 • Hakikisha unaelewa kila kitu katika mkataba wa upangaji kabla ya kutia saini.
 • Pata maelezo ya mwenye nyumba au mawasiliano.
 • Wamiliki wa nyumba wengi watakuuliza kulipa dhamana. Kama unashindwa kuzingatia nyumba vizuli, kuharibu au una deni ya kodi mwishoni mwa upangaji wako, mwenye nyumba yako anaweza kudai baadhi au yote ya dhamana.
 • Kama mwenye nyumba wako anachukua dhamana, ni lazima:
 • Wasiliana na Residential Tenancies Bond Authority kama hupokeyi risiti ya dhamana ndani ya siku 15 ya malipo.
 • Risiti ya dhamana yako ni muhimu - usiyipoteze. Wakati wa mwisho wa upangaji wako utahitaji risiti ili kuomba dhamana nyingine.
 • Mwenye nyumba yako au Shilika yako lazima wakupatie karatasi mbili ambaye zimesainiwa za ripoti ya hali ya nyumba kabla ya kuhama. Angalia nyumba ni salama na uwaambie mwenye nyumba yako au shirika yako taarifa ambaye inaweza kureta hatari, kama vile uhaba wa uzio wa pool au matatizo ya dhahiri ya umeme. Kukagua nyumba na kujaza katika ripoti, andika uharibifu wowote upo kama vile nyufa, alama juu ya kuta, au kuvunjika kwa mlango. Pia kumbuka juu ya ripoti ya hali ya nyumba kama hukubaliani na chenye mwenye nyumba au shirika wameandika.
 • Rudisha nakala moja ambaye imesainiwa kuhusu ripoti ya hali ya nymba kwa mwenye nyumba au shirika kwenye siku tatu kabla ya kuhama.
 • Zingatia nakala ya ripoti ya hali ya nyumba. Unaweza kuyihitaji mwishoni wa upangaji wako kama kuna ubishi kuhusu nani anapaswa kulipa kwa ajili ya kusafisha, uharibifu, au badala ya vitu vimekosa.
 • Wasiliana na makampuni ya maji, umeme, gesi na simu kwa uchaguzi wako na kuhakikisha kwamba vinatumika wakati unahama. Kwa ujumla, ni wajibu wako kuandaa huduma hizi na kulipa bili.

Wakati wa upangaji

Una haki na majukumu fulani wakati wa kukodi nyunmba.

 • Lipa kodi yako kwa wakati. Una haki ya kupokea risiti kwa malipo ya kila kodi.
 • Zingatia nyumba iwe safi. Kama huna, au hukuharibu nyumba, unaweza kupata dhamana kamili nyuma wakati wewe unamaliza upangaji.
 • Usikarabati au kubadilisha nyumba bila ridhaa ya mwenye nyumba.
 • Heshimu majirani kwakuwapatia amani na faragha na kuhakikisha wageni wako wanafanya hivyo.
 • Mwenye nyumba yako au Shirika ana haki ya kuingia kwenye nyumba, lakini ni lazima kutoa taarifa angalau ya masaa 24 katika kuandishi na kukuambia kwa nini wanahitaji kuingia kwenye nyumba hiyo. Sababu halali inatajwa kwenye karatasi yetu ukurasa kuhusu mwenye nyumba au mmiliki. Wanaweza pia kuingia nyumba wakati na tarehe muliokubaliana, muda usiyo mrefu wa zaidi ya siku saba baada ya makubaliano.
 • Mwambie mwenye nyumba yako au shirika kuhusu matengenezo yoyote atakiwa kukarabatiwa.

Matengenezo ya haraka

 • Wasiliana na mwenye nyumba yako au shirika kama unahitaji matengenezo ya haraka. Matengenezo ya haraka ni mambo ambayo yanafanya nyumba isiwe salama au hawawezi kuiishi katika nyumba hiyo, kwa mfano, uharibifu wa uzio ya pool, vifaa vya umeme au Mashini ya kureta joto, kupasuka kwa maji, nyumba kuvuja, kuvuja kwa gesi au kuvunjwa kwa choo. Unaweza kupata orodha kamili juu ya matengenezo wetu kwenye Ukurasa wa matengenezo ya haraka.
 • Mwenye nyumba au shirika lazima kujibu mara moja ombi kwa ajili ya matengenezo ya haraka.
 • Kama huwezi kupata majibu ya haraka kutoka kwa mwenye nyumba yako au shirika, unaweza kuidhinisha kukarabati kwa pesa hadi ya $1800. Weka risiti zote na rekodi ya majaribio yako kwa kupanga matengenezo ya haraka.
 • Unaweza kisha kutoa kwa mwenye nyumba yako au shirika wakurudishie pesa ulilipa kwa ajili ya gharama za matengenezo ya haraka. Wana siku 14 ya kukulipa kutoka kwenye tarehe waliyopokea ilani. fomu zinapatikana kwenye ukurasa wa mafomu na utangazaji.
 • Kama huwezi kulipa kwa ajili ya matengenezo ya haraka, gharama za matengenezo ni zaidi ya $1,800 au mwenye nyumba anakataa kulipa, piga Consumer Affairs Victoria kwa ushauri.

Matengenezo yasiyo ya dharura

 • Unaweza kuomba kwa ajili ya matengenezo yasiyo ya dharura kwa mwenye nyumba yako au shirika kwakuandika. Unaweza kuandika barua au barua pepe au kutumia aina inapatikana kutoka ukurasa wa mafomu na utangazaji.
 • Zingatiya habari ya kila barua, barua pepe, ujumbe wa maandishi, fomu na ripoti, ili kwamba kama kuna tatizo au mgogoro, una ushahidi wa matendo yako yote na maombi.
 • Ita Consumer Affairs Victoria kama mwenye nyumba au shirika haijafanya matengenezo ndani ya siku 14 ya kupewa taarifa.

Kumaliza kupanga

Wakati unataka kuhamia kwenye nyumba unayokodi, lazima kutoa kwa mwenye nyumba yako kiasi sahihi ya taarifa na kuacha nyumba hali safi.

 • Mwambie mwenye nyumba yako au shirika wandikiye wakati anataka kuondoka.
 • Angalia na Consumer Affairs Victoria kujua ni kiasi gani cha mda unalazimisha kutoa. Hii itatofautiana kulingana na hali yako.
 • Jadili kurudisha dhamana na mwenye nyumba yako au shirika.
 • Jaza fomu ya dhamana ya madai na yirudishe kwenye Residential Tenancies Bond Mamlaka. Fomu lazima iwe na saini ya wewe na mwenye nyumba yako au shirika.
 • Usisaini fomu ya dhamana ya madai kama hukubaliani na kiasi gani cha dhamana mwenye nyumba anadai. Wasiliana na Consumer Affairs Victoria kwa ushauri wa bure.
 • Kamwe usisaini fomu tupu ya dhamana ya kudai.
 • Lipa kodi yoyote ya kodi ya nyumba na mabili.
 • Safisha nyumba na chukua vitu/mali yako yote na wewe.
 • Zingatia ripoti wakati wa kesi ya mgogoro.
 • Acha anwani ya kuwasiliana na namba ya simu na mwenye nyumba yako au shirika.

Mambo muhimu yakukumbuka

 • Usisubutu kusaini kitu chochote isipokuwa unaerewa nini maana yake.
 • Kamwe usisaini fomu tupu, hata kama inaonekana rasmi.
 • Zingatia fomu za kitu chochote unasaini.
 • Uliza risiti kila wakati una unalipia kitu fulani.
 • Zingatiya risiti ya dhamana yako na risiti nyingine zozote za kodi ya nyumba au matengenezo katika mahali salama.
 • Kutafuta ushauri wa bure kutoka Consumer Affairs Victoria kama una tatizo ya kukodisha au unaswali.

Videos

Kuanzi na kumaliza upangaji